Naogopa mimba kuliko corona- msanii Akothee akiri

Muhtasari
  • Msanii Akothee akiri kitu ambacho anaogopa wakati huu wa sasa, kuliko corona

Kwa kweli nani hamfahamu msanii Esther Akoth almaarufu Akothee humu nchini, kwa ajili ya sifa zake tofauti.

Wengi wanamfahamu kama 'president of single mothers'. kwa ajili ya kukuza watoto wake pekeyake.

Msanii Akothee ana hadithi ya kusisimua kuhusu safari yake ya usanii, na hata ya kuwa mzazi.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrama Akothee alikiri kwamba anaogopa mimba kuliko virusi vya corona.

Huku akiendelea kusimulia Akothee alisema kwamba corona unaweza ambukiza watu wasipovaa maski.

Msanii huyo aliwashauri mashabiki wake waache abebe mimba kwenye ndoto kwa maana wanaume wa siku hizi wamekuwa wakiteleza kama sabuni.

"Niacheni Nibebe mimba kwenye Ndoto tafathali, kila mtu amekubaliwa kuota ,niacheni note 😂😂😂😂🤦🤦Mimba yaweza kufanya ukawa mlevi hata KWA kunywa maji tuu.😂💃💃💃💃💃💃." Aliandika Akothee.

Kwa kweli wewe unaogopa nini maishani, tayari madam boss ameweka wazi nini haswa anaogopa wakati huu.