Orodha ya wasanii bora mwaka wa 2021(Maoni)

Nadia-2-e1566897594626-696x395
Nadia-2-e1566897594626-696x395

Tasnia ya muziki kwa mara nyingine imeonekana kuinuka kwa mara tena baada ya wasanii tofauti kujitolea na kutoa vibao vipya kila kuchao.

Kuna baadhi ya wsanii ambao wamewafurahisha mashabiki wao kwa ajili ya bidii ambayo wanayo katika kazi yao.

Lakini je kulingana na maoni yako nani anapaswa kuwa msanii bora mwaka wa 2021 kati ya wasanii hawa.

 

1.Nadia Mukami

Ni msanii wa kike ambaye ameonyesha bidii kubwa kwenye tasnia ya usanii licha ya yake kuwa mwanamke.

Nadia amekua akitoa kibao kimoja baada ya kingine huku akiwashirikish wasanii wenzake.

2.Otile Brown

Amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda sasa huku akitoa kibao kimoja baada ya kingine.

Otile Brown
Otile Brown

Mapema wiki jana Otile alitoa kibao cha siku ya wapendanao yaani 'Valentines'.

3,Mejja

 

Msanii Meja mtoto wa Khadija amekuwa akivuma kila mara endapo kibao kipya kimetolewa, amekuwa kwa tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka kumi sasa, hivi majuzi Mejja ametoa kibao ambacho kinafahamika kama 'Ulimi Wangu'.

Mejja na Massawe Japanni studioni
Mejja na Massawe Japanni studioni

4.Willy Paul

Ni msanii ambaye amekuwa akisonge na mbele licha ya kupokea ukosoaji mkubwa na kejeli kutoka kwa mashabiki.

Tumemuona hivi majuzi akiwa amemsajili msanii katika lebo yake na kutoa kibao kipya.

Willy Paul
Willy Paul

Swali kuu ni je ina maana wasanii wa kike wamelemewa na kazi hii ya usanii au wapo wapi?

Kulingana na maoni yako ni msanii yupi ambaye ameanza vyema mwaka huu na anapaswa kuwa msanii bora wa mwaka wa 2021.