Watu wanadhani kwamba wananijua, lakini hawanijui-Huddah Monroe

Muhtasari
  • Kulingana na Huddah katika maisha yake ya kawaida ana marafiki wengi kama vile anao kwenye mitandao ya kijamii
Huddah 1
Huddah 1

Mwanasosholaiti na mwana biashara Huddah Monroe ameweka wazi kwamba watu ambao wanadhani wanamjua hawamjui.

Kulingana na Huddah katika maisha yake ya kawaida ana marafiki wengi kama vile anao kwenye mitandao ya kijamii.

Huddah alisema sababu ya kuwa na marafiki chache katika maisha yake ni kwa ajili ya kuwaambia ukweli katika maisha yao.

 

"Watu wanadhani  wananijua, ninaweza ishi na wewe kwa miaka 200, na hutawahi nijua, asilimia 90 vitu ambavyo na kuambia ni uongo

Labda itaenda kukusaidia na kukuza," Alisema Huddah.

Mwanabiashara huyo alifichua na kusema licha ya yake kuwapa watu ushauri na kuwasaidia kuna wale wamechukulia hilo kuwa unyonge wake,

"Huwa n shauri kila mtu nimetangamana naye, na kuwaambia ukweli hiyo ndio sababu nina marafiki wachache 

Ninasaidia watu sana mimi si mwenye tamaa,nikiona  uwezo wako nitakuambia na kukusaidia lakini sitatarajia kitu

Baadhi ya watu hao hufikiria kuchua faida yangu kwa maana niliwapa mawaidha,ushauri na kuwasaidia lakini kile hawajui huwezi shinda mwalimu wako

Nilikupa mwongozo na wala si kitabu chote,"