Msanii King Kaka aeleza sababu ya kuwashirikisha wanawake wenye mwili mnene kwenye video yake

Muhtasari
  • Msanii King Kaka aeleza sababu ya kuwapakia wanawake wenye mwili mkubwa kwenye video yake
  • Pia alisema kwamba licha yao kukejeliwa wengine wetu ni akina mama zetu, wapenzi, na hata dada zetu
king kaka-2
king kaka-2

Msanii King Kaka anafahamika kwa kazi na bidii ambayo anatia katika kazi yake ya usaniina hata kupenda mkewe na wanawe.

Wikendi iliyopita King Kaka alivuma baada ya kushirikisha wanawake wenye mwili mnene kwenye video yake.

Huku akipeana na kufichua sababu yake ya kufanya hayo alisema wanawake kama hao wamekuwa wakikejeliwa sana kwenye mitandao na hata jamii zetu.

 

Pia alisema kwamba licha yao kukejeliwa wengine wetu ni akina mama zetu, wapenzi, na hata dada zetu.

Msanii huyo aliwashauri wanaokejeli wawache kitendo hicho kwani sisi sote tuko sawa.

"Acha niwe mkweli asubuhi ya leo. Nilichagua kuweka wanawake wenye ukubwa zaidi kwenye video ya 'Utanipata' kwa sababu wao ni sehemu ya jamii yetu, ni marafiki wetu, dada zetu, marafiki wetu wa kike, mama zetu.

Hivi kwanini wasiwe kwenye video ya muziki ?? Kwanini ??? Tuwache ujinga. Nimeona wahusika wengine wakiwashambulia kwa uzito wao, Ati kwanini wapo?

Wakati tunagundua kuwa sisi wote ni sawa na wanadamu basi kila kitu kitakuwa na maana. Labda huwezi kujua ni nini mtu anapitia na athari zake zinaweza kuwa nini.

Unganisha kwenye Bio. Acha aibu ya mwili, Tuwache siasa na Ujinga." liandika KIng Kaka.

Pia kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram pia alipakia ujumbe wa mmoja wa wanawake ambaye alisema kwamba kuna rafiki yake ambaye alikataa asimamie harusi yake kwa maana yeye ni mnene.