(+Video) Sina uhusiano wa kimapenzi na Betty Kyalo-Alinur aweka mambo wazi

Miezi chache iliyopita mwanasiasa Alinur alivuma kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanabiashara Betty Kyallo.

Akizungumzia suala hilo alkiwa kwenye mahojiano na Radiojambo, aliweka wazi kwamba yeye ni mshauri wa Betty wala si mpenzi wake.

Alinur Pia alisema kwamba ni mume na baba wa watoto wawili.

"Mimi ni baba wa watoto wawili, nilikuwa nashinda na Betty Kyallo, kwa maana mimi ni mshauri wake, nadhani anataka kuwania kiti cha mwakilishi  wa wanawake kaunti ya Nairobi

Jina la 'Somali bae' lilitoka baada ya uvumi kuenea kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na Betty, kwa kweli si kuhisi vibaya kuitwa hivyo lakini nilikana madai hayo

Sina uhusiano wa kimapenzi na Betty Kyallo, nimekuwa nikimshauri katika sekta ya siasa," Alielea Alinur.

Huku akizungumzia jinsi mkewe alichukulia madai hayo alisema haya,

"Baada ya mke wangu kuona habari hizo aliniita na kuniuliza ni nini inaendelea nilimwambia ukweli

Unajua watu wengi wamekosa kazi sasa wanaenda kwenye mitandao ya kijamii na kusema mambo ya uongo

Sijali ambacho watu wanasema kwa sasa,"

Hii happa video ya mahojiano hayo;