Ata uhusiano ukiisha kwa machozi ni yako? Zari Hassan awauliza wakosaoji wake

Muhtasari
  • Zari Hassan awatupia wakosoaji wake vijembe baada ya kukosoa uhusiano wake na mpenzi wake
Zari Hassan

Mwanabiashara Zari Hassan kwa muda sasa amekuwa akivuma kwenye mitandao ya kijamii, hii ni bada ya kumtambulisha mpenzi wake mitandaoni.

Baadhi ya wanamitandao walimkejeli huku wengine wakimpongeza kwa hatua yake.

Zari amekuwa akikabiliana na kejeli ipasavyo, huku akiwajibu wakosoaji wake ambao wamekuwa wakikejeli uhusiano wake aliwaambia hata uhusiano wake uishe kwa machozi si ya mtu yeyote.

 

Pia alisema kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawapendi wenzao wakiwa na furaha katika maisha yao.

“Hata ikiishia kulia ni machozi yako? Vizuri itakuwa na sherehe ya machozi baada ya hayo. Hakika watu wanapenda taabu; unachukia kuona wengine wakiwa na furaha. Vizuri ni nzuri kwangu," Aliandika Zari.

Zari alifahamika sana baada ya kuwa mpeni wake staa wa bongo Diamond Platnumz ambaye walichumbiana kwa muda na kisha wakaachana.