Maisha ya kila mtu yana misimu wakati wako ukifika ng'aa-Ushauri wake Grace Ekirapa

Muhtasari
  • Grace na mumewe Pascal Tokodi hawajakuwa na aibu wakizungumzia ndoa yao, wala changamoto wamepitia awali kabla ya umaarufu wao
  • Grace alisema kwamba maisha ya kila mtu yana misimu wake
Grace Ekirapa

Mtangazaji Grace Ekirapa kupitia kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ya instagram amekuwa akiwapa mashabiki wake nguvu na ushauri wa kuendelea na maisha.

Grace na mumewe Pascal Tokodi hawajakuwa na aibu wakizungumzia ndoa yao, wala changamoto wamepitia awali kabla ya umaarufu wao.

Kupitia kwenye ukurasa huo huo aliwashauri mashabiki wake kama wakati wa mtu wa kung'aa umefika anapaswa kung'a kulio awali.

 

Pia alisema kwamba kuna wale hutumia wakati kujaribu kupunguza mwanga wa watu wengine kwa sababu tu wanaogopa kung'arisha wao wenyewe.

Grace alisema kwamba maisha ya kila mtu yana misimu wake.

"Maisha ya kila mtu yana misimu. Wakati  wako ukifika, ng'aa kama hapo awali. Usifiche taa yako kwa sababu mtu fulani anatishwa nayo

Watu wengi hutumia wakati kujaribu kupunguza mwanga wa watu wengine kwa sababu tu wanaogopa kung'arisha wao wenyewe

Kumbuka, msimu huo utapita, kwa hivyo fanya sasa au milele ubaki kuwa kivuli nyuma ya nuru ya watu wengine

Zingatia pia kung'arisha na usijali ni nani taa  yake ni nyepesi kuliko yako au nani utazima taa yake kwa sababu hiyo ni kazi mingi ️ Kuwa na siku ya kung'aa 😊😊," Aliandika Ekirapa.

Swali kuu ni je umechukua msimu wako wa kung'aa au umeacha umekupita?