Nilichukia macho yangu kwa maana ni makubwa-Muigizaji Nyce wanjeri

Muhtasari
  • Katika kila mwili wa mwanadamu kuna sehemu au kiungo cha mwil ambacho huona Mungu hakufanya vyema na kukichukia
  • Nyce alisema kwamba alikuwa anachukia Macho yake kwa maana ni makubwa, kwani hakujua yatakuja kuwa faida kwake wakati wa uigizaji
Shiro-Auntie-Boss
Shiro-Auntie-Boss

Katika kila mwili wa mwanadamu kuna sehemu au kiungo cha mwil ambacho huona Mungu hakufanya vyema na kukichukia.

Baadhi ya wasanii, waigizaji kupitia kwenye kurasa zao za instagram wamekuwa wakizungumzia kiungo ambacho wanachukia au walikuwa wanakichukia walipokuwa wakikua.

Muigizaji Nyce wa Njeri almaarufu Shiro, alifahamika kupitia kwa uigizaji wake katika kipindi cha 'Auntie Boss'.

Nyce alisema kwamba alikuwa anachukia Macho yake kwa maana ni makubwa, kwani hakujua yatakuja kuwa faida kwake wakati wa uigizaji.

"Nilichukia macho yangu kwa maana ni makubwa, na nilikuwa aaah okey mimi bado ni mwembamba sasa ni mali yangu katika uigizaji," Aliandika Nyce.

Pia muigizaji ambaye anafahamika sana kama Monica, Brenda Wairimu aliweka wazi kwamba alichukia midomo yake lakin baadaye ilikuja kuwa faida kwake.

"Nilichukia midomo yangu ikikua,mwishowe ilikuwa sababu yangu ya kupata kazi hii, kuna unzo hapo na mahali," Aliandika Brenda Wairimu.

Somo kuu au jambo kuu la kujifunza ni kwamba hata kama unachukia nini katika mwili wako, kumbuka kuna sababu ambayo Mungu alikuumba jinsi ulivyo.