Sisi ni marafiki wazuri hata baada ya kuachana na Joyce-Tony Kwalanda afunguka

Muhtasari
  • Mwaka jana Muigizaji Joyce Maina na Tony Kwalanda waliua sana mwaka jana baada ya Kwalanda kumvisha Joyce pete ya uchumba
  • Wawili hao wamevuma tena siku chache zilizopita baada ya Joyce kuweka wazi wameachana

Mwaka jana Muigizaji Joyce Maina na Tony Kwalanda waliua sana mwaka jana baada ya Kwalanda kumvisha Joyce pete ya uchumba.

Wawili hao wamevuma tena siku chache zilizopita baada ya Joyce kuweka wazi wameachana.

Huku Kwalanda akiwa kwenye mahojiano aliweka wazi kwamba hata baada ya kuachana na Joyce bado wao ni marafiki wa karibu na huwa wanawasiliana.

 

"Tulikuwa na tofauti zetu kwenye uhusiano wetu lakini, tulikaa chini na tukasuhuhisha, nataka kuwashauri wananchi kama uhusiano wenu uko na shida na hamuwezi suluhisha heri juachane kabla ya mambo yaharibike

Sisi ni marafiki wazuri sana, huwa tunawasiliana na tunafanya kazi katika kituo kimoja,tulikuwa na uhusiano ambao umekomaa

Najua mambo mengi uhusu Joyce na anajua mambo mengi kunihusu,tulikuwa tunaongea ukweli katika uhusiano wetu

Nilisoma na kujifunza mambo mengi kutoka kwake, na huwa namtakia mazuri na mafaniko katika maisha yake

Nikisikia mtu amemguza Joyce vibaya nitauja na jeshi," Alisema Kwalanda.

Akizungumzia kuhusu kuchumbia mwanamke mwingine, na mwenye umri wa miaka 24, alikana madao hayo na kusema kwamba walipatana kwenye shehere na kuchukua piacha hiyo.

"Wanawake hufurahi sana wakipatana na mtu mashuhuru, na unaeza chukua picha, ghafla aliweka kwenye mitandao picha zetu, na hadithi zikaanza

 

Mimi naweka mambo wazi mwanamke huyo sio penzi wangu, na kwa sasa sina mpenzi yeyote, ni vile tulikuwa katika sherehe ya mtu na watu wakalewa na mambo yakatendeka hivo tu,"

Hii hapa video ya mahojiano hayo;

#TonyKwalanda #JoyceMaina #CelebrityCheck #KatanuMunyao