"Lazima afikishwe mahakamani!" Msanii Harmonize atishia kumshtaki Rayvanny

Muhtasari
  • Msanii Harmonize ametishia kumshtaki msanii mwenzake Rayvanny, kwa yale aliosema kumwaribia jina na jina la lebo yake
  • Harmonize ameorodhesha baadhi ya watu ambao watakao enda kwenye mahakama
hamo 3
hamo 3

Msanii Harmonize ametishia kumshtaki msanii mwenzake Rayvanny, kwa yale aliosema kumwaribia jina na jina la lebo yake.

Msanii huyo aliahidi kwamba atamlipa milioni ya pesa kama hilo ndilo litafanya achunge jina lake na kuwa hana hatia.

Harmonize ameorodhesha baadhi ya watu ambao watakao enda kwenye mahakama, kwa ajili ya kumwaribia jina kupitia kwa video waliopakia kwenye mitandao ya kijamii.

 

Katika video hiyo Harmonize anasikika akizungumza akiwa kwenye bafu na mwanamke.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema kwamba wale ambao watafika mahakamani itawagharimu kumlipa kama faini ili iwe mfano na funzo kwa wau wengine.

"Taarifa Kwa Umaa ...!!! 📢 Video Zilizo tengenezwa na Kusambazwa Mtandaoni Zikiwa Zinaonyesha Sura Yangu Na Kuunganishwa Na Utupu Wa Mtu Mwingine Kisha Kuunganishwa Na Sauti Yangu Kwa Lengo La Kunichafua Kunidhalilisha Na Kuharibu BRAND YANGU ambayo Nimeitengeneza Kwa Mabilioni Ya Shiringi ..!!!! Itoshe tu Kusema (1) Sio Mimi ...!!Narudia Sio Mimi na Sina Maumbile Yale ..!! (2) Hiyo Video Ninayoongea Kwa Sauti Nikiwa Bafuni Nilikuwa naongea Na Mtu Niliekuwaga Nae Katika Mahusiano Ni Kwaida Mtu Kuzungumza na Mtu wako Wakati Wowote Mahala Popote Sitaki Kujua Alietengeneza Ni Nani Au Kaipataje ila Ninachosema ni Kwamba YEYOTE Alie Husika na Hili Swala Linalolenga Kunichafua Na Kuni zalilisha LAZIMAAAA NARUDIA LAZIMAAAA ...!!! Atafikishwa Mahakamani Ili kukomesha CHUKI & NA TAMAA zinadho Athiri watu wasio Kuwa na Hatia ...!!!" Aliandika Harmonize.

Alisisitiza kwamba baadhi yao wameharibu lebo yake ambayo alitengeneza na pesa nyingi.

"Hiyo Unayoiona Hapo Ni orodha Fupi Ya Majina Ya Watu Ambao Penginepo Hutowaona Tena Hapa (INSTAGRAM) Watanilipa (FINE KUBWAA) ikiambatana Na Kifungo Juuuu Ili IWE MWIKO kama Sio Mfano MAANA SHERIA ITAFWATA MKONDO 🙏 JOPO LA WANASHERIA WANGU WAPO KAZINIII 🐘,"