'Nilisaini kile kilihitajika kusainiwa,'Anerlisa Muigai aweka mambo haya bayana

Muhtasari
  • Anerlisa aweka wazi wametalikiana na Ben Pol
  • Pia alisema kwamba anaweka mambo wazi hataki kamwe kuhusishwa na mtu yeyote

Anerlisa Muigi kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram alifichua kwamba aliti saini makaratasi ya talaka kati yake na Ben Pol.

Kupitia kwenye mitndo hiyo Muigai alisema kwamba kile kilihitajika kufanyika kimefanyika na ametia saini.

Pia alisema kwamba anaweka mambo wazi hataki kamwe kuhusishwa na mtu yeyote.

Alisema kwamba jambo la muhimu maishani mwake sasa ni kazi yake, na amani katika maisha yake.

"Nataka kuweka mambo wazi kuwa nilisaini chochote  kilichohitajika kusainiwa, na sitamani kuhusishwa na mtu yeyote

mtazamo wangu hivi sasa, ni kazi yangu na amani yangu," Aliandika Anerlisa.