'Nyota wangu ulizaliwa kuangaza,'Tanasha Donna amwandikia mwanawe ujumbe wa kipekee

Muhtasari
  • Tanasha Donna amwandikia mwanawe ujumbe wa kipekee
Diamond na Mwanawe Naseeb Junior aliyempata na Tanasha Donna

Ni furaha ya kila mzazi kumuona mwanawe akiwa anaendelea vyema katika maisha yake kutoka hatua moja hadi nyingine.

Msanii Tanasha ni mama mwenye furaha moyoni mwake kwa ajili mwanawe anakuwa kutoka kwa hatua moja hadi nyingine.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia picha ya mwanawe na kumwamndikia ujumbe wa kipekee huku akimwambia alizaliwa kuangaza.

 

Pia alisema kwamba mwanawe ni nyota wake na anampenda sana.

"Mama anapenda wewe  @ naseeb.junior. Mwenyezi Mungu akubariki pamoja na njia yako &na uweze kukua kuwa mwenye busara mwana ... na uweze kufanya kila wakati na kufuata njia yako mwenyewe Nyota yangu. Mzaliwa wa kuangaza ... ⭐👶🏽❤️," Aliandika Tanasha.

Baba yake Naseeb Junior ni mwanawe staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platnumz.

Tanasha na Diamond waliachana mapema mwaka jana.