'... Mnaona matokea,'Khaligraph Jones ajisifu baada ya uamuzi wake Uhuru Kenyatta

Muhtasari
  • Khaligraph Jones ajisifu baada ya uamuzi wake Uhuru Kenyatta
  • Kuna wale walisema kwamba anakubali kutumiwa na wanasiasa badala yake kuzingatia kazi ya usanii wake
khali-e1471415170725
khali-e1471415170725

Siku chache zilizopita rappa na msanii wa nyimbo za Hip Hop Khaligraph Jones maarufu Papa Jones amekuwa akipokea kejeli na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wasanii wenzake na wanamitandao baada ya kuwa na mkutano na naibu rais William Ruto.

Kuna wale walisema kwamba anakubali kutumiwa na wanasiasa badala yake kuzingatia kazi ya usanii wake.

Siku ya sikukuu ya Labour day Rais Uhuru Kenyatta alifungua baa, huku Jones akijilimbikizia sifa kwa uamuzi wake rais.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikuwa na haya ya kusema;

"Baada ya mkutano Wangu na Serikali Wiki iliyopita, nina uhakika kwamba mnaona matokeo, sio yote ambayo tulikuwa tumetarajia lakini jambo hilo limeanza

Sasa nishukuruni," Aliandika Jones.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya msanii huyo kujisifu;

redsanmusic: Omolo una onea hio tyre brathee. πŸ’ͺ🏾

morrison_litiema: Look ni safiπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

sod_ium._Ngorii:  my GπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯❀️

 
 

sod_ium._: You did it G

renylusava57: Shukran OG...you shall be respected...luku ni motooooooπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

jamstamusic: Sasa ndio Kasheshe zitaanza... And legends will be reborn.... 😍😍πŸ”₯πŸ”₯

_faded_sushii: Respect the OGπŸ€žπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

dee_kiige: Hii government yako though πŸ˜‚πŸ˜‚

Kwa muda sasa tasnia ya burudani imedhoofika kutokana na janga la corona,baada ya maeneo ya burudani kufungwa ili kudhibiti msambao wa virusi vya corona.