Hakuna siku watoto wangu walikosa walichotaka,'Mchekeshaji Professor Hamo ajibu madai ya kutowasaidia wanawe

Muhtasari
  • Mchekeshaji Professor Hamo ajibu madai ya kutowasaidia wanawe
  • Jemutai alifichua kwamba walipatana na Hamo kwenye kipindi cha Churchill ambapo walianza uhusiano wa kimapenzi licha ya Hamo kuwa na familia
images
images

 Mchekeshaji wa churchill Professor Hamo na mcheshi Jumutai wamevuma sana baada ya mwanablogu Edgar kufichua kwamba mchekeshaji huyo hawasaidii wanawe.

Jemutai alifichua kwamba walipatana na Hamo kwenye kipindi cha Churchill ambapo walianza uhusiano wa kimapenzi licha ya Hamo kuwa na familia.

Mcheshi hyo alisema kwamva anahitaji msaada kwani hana pesa za kulipa kodi ya nyumba na baba wa watoto wake hawasaidii.

 
 

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram wa Hamo,amekana madai hayo na kusema kwamba hamna siku hata moja wanawe walilaal njaa wala kukosa walichohitaji maishani.

Pia alifichua kwamba mkewe ndiye huwatumia msaada wanawe ambao haishi na wao.

"Najua meni yamesemwa lakini nataka kuweka mambo bayana kwa mashabiki wangu, nina watoto ambao naishi nao na ambao hawaishi na mimi

Nimekuwa nikiwasaidia wanangu tangu siku ya kwanza na hamna siku ambayo walikosa chakula wala mahali pa kuishi ama kile walitaka

Mkewe wangu ndiye huwa anatuma pesa kwa watoto ambao hawaishi na sisi, haya yamekuwa makubaliano kati ya familia yangu na mama wa watoto wangu," Alisema Hamo.

Kupitia kwa ujumbe mwingine mchekeshaji huyo alidai kwamba anaamini watoto wanahitaji mazingira yenye utulivvu wanapokua.