'Hamo aliona watoto wake mwisho mwaka jana Oktoba,'Jemutai amshambulia Hamo

Muhtasari
  • Mcheshi Stella Jemutai Koitie ametupilia mbali madai ya Professor Hamo kwamba huwa ana wasaidia wanawe
jemutaionstage
jemutaionstage

Mcheshi Stella Jemutai Koitie ametupilia mbali madai ya Professor Hamo kwamba huwa ana wasaidia wanawe.

Awali kwenye ukurasa wake Hamo wa instagram aliweka wazi kwamba huwa anawasaidia wanawe, na kuwa mkewe ndiye hutuma pesa.

Kupitia kwenye ukurasa wake Jemutai wa facebook, alitupilia madai hayo na kusema kwamba mara ya mwisho mchekeshaji huyo kuona wanawe ilikuwa mwaka jana Oktoba.

 

Pia Jemutai amedai ya kwamba anamheshimu sana mkewe Hamo licha ya hayo yote.

Huu hapa ujumbe wake Jemutai;

"Ni siku ya Jumapili kwa mapenzi yake Mungu, kwanini tunadanganya mapema hivi, kwanza mra ya mwisho Hamo kulipa kodi ya nyumba ilikuwa mwaka jana Okotoba na kutoka hapo aliacha kupokea simu za mwenye nyumba

Na mheshimu Mama Melisa sana lakini kwa maana umeamua kumleta kwa haya, pesa ambazo alinitumia ni elfu 9 pekee

Wakati wa kwanza alituma elfu 2 wakati mtoto JJ alikuwa mgonjwa, mara ya pili alituma elfu 2 wakati sikuwa na pesa za chakula na elfu 5 alituma juzi wakati kila kitu ilikuwa hadharani,"

Pia alidai aliwaona wanawe mwaka jana, na wakati mwingine alikuja usiku wa manane akiwa mlevi huku akishindwa ni watoto wagani huwa wameamka usiku wa manane.

"Wakati wa mwisho Hamo aliona watoto wake ambao ni Jeremy na Kaylee ilikuwa mwaka jana Oktoba kabla ya kutoka kwangu

 

Tangu siku hiyo amekuja kwangu mara nne wakati wote usiku ni wakati mmoja alikuja saa nne asubuhi,mwezi jana alikuja saa nane usiku, na nyakati hizo zote alikuja akiwa amelewa chakari

Watoto wagani ukuwa wameamka saa nane asubuhi, mwanamume mwenyewe anakuja bila hata maziwa wakati wa mwisho alikuwa na Oreos mbili

Hamo afadhali jua ya kwamba nimeficha mengi yasiwe hadharani, na hata wakati ambao ulileta vurugu na ukaomba msamaha Abner,"