'Lazima Niende Njia Yangu Na Wewe Uende Njia Yako,'Weezdom atoka katika lebo ya EMB

Muhtasari
  • Meneja wa msanii Bahati,Weezdom atoka kwenye lebo ya EMB

Meneja wa msanii Bahati, Weezdom kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kwamba ametoka katika lebo ya EMB inayomilikiwa na msanii huyo.

Weezdom alimshukuru msanii Bahati kwa kumpa kazi yenye heshiima huku akisema kwamba amemsaidia kwa kutoa nyimbo zake ana anamatumaini atazidi na bidii yake.

"Niaje Watu Wangu? Huyu Msee Mnaniona Hapo Na Yeye Ni Beshte Yangu Sana Anaitwa BAHATI na Tumetoka Mbali Sana Na Yeye, Tumekosana Na Yeye kabla Na Tukaskizana

Nafurahia Vitu Anafanya, Pamoja TumeFanya Vitu Deadly, Tumebadilisha ulimwengu, Nimemsaidia Kutoa nyimbo zake kwa watu na kama meneja wake nashukuru Mungu Alinipea alinipa kazi ya msanii ambaye anaheshimika sana nchini na nikafanya kazi yangu Ata Mungu anajua nimefanya kazi yangu

Lakini inafika wakati maisha ya mwanadamu Lazima afanye mambo mengine kwa hivyi ndugu yangur Bahatinajua una miradi ambayo inakuja Na natumai Mungu Bado Ataendelea Ku'Administer Vitu Great From Wewe To The People It's Only That Now Hii Ni Ile Junction Lazima Niende Njia Yangu Na Wewe Uende Njia Yako," Aliandika.

Pia alipongeza timu moya ya Bahati huku akifichua kwamba mssanii huyo anapanga kutoa albamu hivi karibuni.

"And Also I Hope Your New Team Watadeliver Na Wakufikishe Kwa Zile Dreams Zote Tulikuwa Nazo..Congratulations On Your New Upcoming Album And I Wish you Nothing but the BestšŸ™Wasee! So Hio Inamaanisha Sina Job Saa Hii So Mkiskia Mahali Kuna Job, Nishtueni Mazee..Ni Boy Wenu WEEZDOM,"