Mafunzo tunayopaswa kujifunza kutokana na drama ya mcheshi Jemutai na Professor Hamo

Muhtasari
  • Mafunzo tunayopaswa kujifunza kutokana na drama ya Jemutai na Hamo
jemutaionstage
jemutaionstage

Wikendi mchekeshaji wa churchill show Professor Hamo na mcheshi Jemutai walivuma sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya Jemutai kufichua kwamba Hamo hajakuwa akiwasaidia wanawe.

Hamo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikana madai hayo, na kusema kwamba amekuwa akiwasaidia watoto wake.

Madai yake Jemutai yanajiri wakati, wanawake wengi wanalalamika wanaume hawajukumiki .

 

Lakini ni mafunzo yapi ambayo tunastahili kujifunza kutokana na drama hiyo ya wikendi.

1.Wanawake tunapaswa kufahamu kumchumbia mwanamume ambaye ana familia kuna majuto na matokeo yake.

Na maanisha kwamba tunapaswa kuchunguza wanaume hawa vyema ili usije ukajipata katika hali ya kuvunja familia ya wenyewe.

2.Hawanaume hawapaswi kuwa na sababu ya kutojukumika; Lazima kila mwanamume awe na sababu ya kutojukumikia familia yake, lakini wanapaswa kufahamu ya kwamba hawapaswi kuwa na sababu yeyote

3.Msiwafanye watoto wenu wateseke kwa ajili ya ugomvi wenu wawili, wazazi na watu mashuhuri wanapaswa kujua kwamba watoto hawana makosa na hamna mtu ambaye alichagua kuzaliwa au kuja duniani.

4.Kama kuna tatizo kati ya wazazi wawili wanapaswa kutafuta njia yenye amanai ya kutatu shida zao na wala sio kuleta vurugu mbele ya watoto, pia watoto wanahitaji amni.

5.Watu mashuhuri wwanapaswa kuwa mfano mwema kwa nchi nzima na kwa mashabiki wao, kwani kuna wale wanafuata nyayo zao maishani.