Mimi na mapacha tunakupeza sana-Jacqueline Mengi amkumbuka mumewe

Muhtasari
  • Jacqueline Mengi kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliandika ujumbe huku akimkumbuka mumewe Reginald Mengi, miaka miwili baada ya kifo chake

Jacqueline Mengi kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliandika ujumbe huku akimkumbuka mumewe Reginald Mengi, miaka miwili baada ya kifo chake.

Kupitia kwenye ujumbe wake alimshukuru Mungu kwa wakati ambao walikuwa naye, huku akisema yeye na wanawe wanampeza sana.

"Mpenzi wangu, tunamshukuru Mungu kwa wakati tuliokuwa na wewe, kwa upendo wa ajabu uliyotupatia, kwa hekima yako, kwa masomo tuliyojifunza katika uangalizi wako na wale ambao tunaendelea kujifunza kwa kutokuwepo kwako. Mimi na mapacha tunakupeza sana. Endelea kupumzika kwa amani," Jacqueline Aliandika.

 

Mengi aliaga dunia akiwa mjini Dubai, huku mozo wa mali yake ukiendelea hata baada ya kifo chake.

Hizi hapa jumbe za wanamitandao;

Tush: He was such an inspirational personality and I learned a lot from him.

D.G: He was a good man. May he continue resting in peace

Traveladventureman.: We miss him too, our inspiration, our fellow chaggan. May God continue to Rest His Soul In Peace.

Gervas Maiko:  RIP mzee wetu. Tunakukumbuka sana, ulikuwa mtu wa mfano kwa watanzania wa upendo wako kwa watu hasa wasiojiweza.