'Ata Iluminati wako broke,'Akothee amshauri shabiki aliyetishia kuuza roho yake kwa shetani

Muhtasari
  • Msanii Esther Akoth  ni miongoni mwa wasanii ambao wamepitia mengi maishani mwao huku wakitia bidii maishani na kuibuka washindi
  • Kupitia kenye ukurasa wake wa instagram amempa mmoja wa mashabiki wake ushauri wa maisha ambaye alitishia kuuza roho yake kwa Iluminati
  • Kulingana na Akothee ata Iluminati hawana pesa na kwamba anapaswa kuanza kufanya kazi na kutia bidii
akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)

Msanii Esther Akoth  ni miongoni mwa wasanii ambao wamepitia mengi maishani mwao huku wakitia bidii maishani na kuibuka washindi.

Kupitia kenye ukurasa wake wa instagram amempa mmoja wa mashabiki wake ushauri wa maisha ambaye alitishia kuuza roho yake kwa Iluminati.

Kulingana na Akothee ata Iluminati hawana pesa na kwamba anapaswa kuanza kufanya kazi na kutia bidii.

 

Pia alimwambia mafanikio ya watu  ambayo anaona kwenye mitandao ya kijamii ni bidii yao na malengo yao.

"Ata Iluminati wako broke hawanunui roho labda damu, Rafiki yangu acha kujipa shinikizo haitajiki. Mafanikio unayoyaona kwenye mitandao ya kijamii leo, ni ndoto za watu, malengo ya malengo na bidii iliyowekwa kwa zaidi ya miaka 20

Hakuna njia ya mkato ya kufanikiwa, kuna mfumo wa mafanikio 💪. Acha kuzingatia watu wanaokula mavuno yao na ujifunze sanaa uvumilivu na upande mbegu zako

Ibilisi pekee anayeweza kununua roho yako ni Mwizi wa Ibilisi) hii inaweza kukupa pesa haraka, nenda tu uwe gungstar, mwanangu, Nenda moja kwa moja benki na uibe Bilioni 1.." Alimwambia Akothee.

Pia alimwambia kwamba pesa ambazo hajafanyia kazi hazitakata kiu yake wala kumsaidia kwani hajamwaga jasho lake.

"Lakini wacha nikuonye, 👉 Pesa ambazo haujafanyia kazi hazitakata kiu chako kamwe, ninapokutazama, unataka njia ya mkato kuifanya 🤣🤣🤣🤣, mpendwa wangu katika tasnia ya mafanikio hakuna lifti,

ni kesi za kutazama, ikiwa kuna dharura au Sio, unataka kuamka TAJIRI. Mheshimiwa MMM bwana Rudi ukalale. Na amka tena Fungu 🙏 Nyenyenyenye, nataka kuuza roho yangu kwa SHETANI. SHETANI WAPI? Hivo ina maana Mungu wetu hana pesa NKT."