Hizi hapa sababu kwa nini lebo ya msanii Diamond WCB ni bora Afrika mashariki

Muhtasari
  • Staa wa bongo Diamond Platnumz anafahamika sana dduniani kote kwa ajili ya bidii yake katika kazi yake ya usanii
Diamond Platnumz

Staa wa bongo Diamond Platnumz anafahamika sana dduniani kote kwa ajili ya bidii yake katika kazi yake ya usanii.

Bali na msanii huyo kufahamika kwa ajili ya usanii wake pia anafahamika kama mmiliki wa runinga na kituo cha redio cha Wasafi.

Pia ana lebo ya muziki ambayo inafahamika kama Wasafi Records.

Lebo hiyo imewasajili wasanii tofauti nchini Tanzania huku wengi wakionyesha bidii yao na kufahamika sana Afrika Mashariki.

Katika makala haya tutaoa sababu kadhaa kwanini lebo ya WCB ni bora Afrika Mashariki.

1.Imewasajili wasanii bora

Kulingana na data asilimia kubwa ya wasanii wamefahamika kupitia lebo ya WCB,pia baadhi ya wasanii hao wamepokea tuzo tofauti za muziki.

2.Usimamizi wa WCB

Ni usimamizi bora ambao unaelewa wasanii na kushika mkono wasanii chipukizi mpaka wanafahamika na kutooa katika tasnia ya burudani.

Lebo hiyo imetajwa kama moja wapo ya lebo ambazo zimekuza uchumi, wakenya wengi wanapenda wasanii wa lebo hiyo huku wakiwasukuma mbele kwa kutazama miziki yao.

Je ni sababu ipi nyingine ambayo inafanya lebo ya WCB kuwa bora zaidi Afrika mashariki, kwa maana bila shaka tumeona vile wasanii wa lebo wanatia bidii huku baadhi ya wengine wakiwekeza na kufungua lebo zao.