'Pengo lako halitazibika,'Rashid Abdalla amuomboleza baba yake

Muhtasari
  • Rashid Abdalla amuomboleza baba yake, huku akimhakikishia kwamba pengo leke halitazibika

Hamna mtu ambaye hufurahia kumpoteza mzazi wake mzazi au mtu ampendaye na roho yake yote, kwa maana watu hao huwacha pengo kwa jamaa zao, na pengo ambalo haliwezi zibwa na mtu mwingine.

Mwanahabari wa runinga ya Citizen Rashid Abdalla anafahamika sana kwa ajili ya kazi yake ya utangazaji, pia kuna wale wanafahamu mama yake mzazi lakini hawamfahamu baba yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimkumbuka baba yake ambaye alifichua siku kama ya leo na tarehe kama ya leo walimzika baba yake miaka chache iliyopita.

 

Pia aliomba Mungu azidi kumuhepusha na adhabu ya kaburi huku akisema kwamba pengo lake halitazibika.

"Babangu siku kama ya leo tulikuzika... daima ntakukumbuka... pengo lako halitazibika. Mungu azidi kukuepusha na adhabu ya kaburi

Mola akusamehe dhambi zako za siri na dhahiri uwe miongoni mwa watakao kabidhiwa kitabu chao kwa mkono wa kulia. Amin

Endelea kupumzika kwa amani MR Abdalla. #myfathermyfriend #missingyou #rip," Aliandika Rashid.