Rafiki yangu alininyang'anya mpenzi wangu tukiwa 'Photoshoot'-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Mwanamume asimulia jinsi alitemwa na mpenzi wake
  • Sio mmoja au wawili ambao wamevunja uhusiano wao wa kimapenzi wa awali kwa ajili ya marafiki zao

Waogope marafiki hasa wakati wa uhusiano wako wa kimapenzi na mpenzi wako, kwa maana sio wote ambao wanafurahia uhusiano wenu kuna wale wanataka mpenzi wako.

Sio mmoja au wawili ambao wamevunja uhusiano wao wa kimapenzi wa awali kwa ajili ya marafiki zao.

Jamaa mmoja alieleza jinsi mpenzi wake alimtoka kwa sababu zisizoeleweka, huku rafiki wake wa karibu akimchukua mpenzi wake siku maalum ya 'Photoshoot'.

 

"Nilimpeleka mpenzi wangu Photoshoot, nikiwa na rafiki yangu ambaye alikuwa anaendesha gari, mrembo huyo alikuwa na urembo wa kipekee

Tukipigwa picha na mpenzi wangu jamaa huyo alikuwa anapindua sura ni kama amekasirika,niligundua kwamba hakuwa anafurahia nikimkaribia mpenzi wangu

Tuliporudi nyumbani, jamaa huyo alimdanganya mpenzi wangu kwamba nimeoa na nina bibi, mpenzi wangu hakuniamini wala kiniamini lakini aliniacha na sasa wako pamoja," Alisimulia.

Je ina maana wanaume hawana mistari ya kujieleza kwa wanawake bali na kuwanyang'anya wenzao wapenzi wao kwa ujanja ambao haustahili?

Haya basi wanaume kuweni macho.