Wazazi mnaeleza aje watoto kuhusu kifo? DJ Piera Makena auliza wazazi

Muhtasari
  • DJ Pierra awauliza wazazi jinsi ya kuwaeleza watoto wao kuhusu kifo
Screenshot-from-2020-06-25-09_22_12
Screenshot-from-2020-06-25-09_22_12

Mcheza santuri Piera Makena ni mwanamke mwenye bidii ya kipekee, licha ya changamoto hupatana nazo katika kazi yake ka mwanamke.

Pierra amekuwa mfano mwema wa wanawake abao wanatia bidii katika kazi zao bila drama yeyote.

Huku kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwauliza wazazi jinsi ya kuwaambia watoto wao kuhusu kifo, hii ni baada ya rafikiye mtoto wake kuaga dunia.

 

Pia alifichua kwamba umekuwa wakati wake mumu katika kulea kumueleza mwanawe.

Mheza santuri huyo alisema kwamba pia anahumia sana kumuona mwanawe ameumia moyo kwa ajili ya kifo hicho.

"Mnafanya aje wazazi, mnawaeleza watoto wenu aje kuhusu kifi, huu umekuwa wakati wangu mgumu katika maisha yangu ya kulea

Kueleza kifo kwa mtoto wangu,mtu mzuri ambaye alikuwa anamuona kila siku alimsaidia kuendesha baiskeli yake na alimchukulia kama mtoto wake

Inauma kumuona mtoto wangu amevunjika moyo,inauma kwamba tumempoteza jirani mwema, nalia kwa ajili ya wavulana wake wawili na familia yake

Sijui jinsi ya kupambana wala kueleza kifo, lala salama Allan," Aliandika Makena.