Wewe ni jua langu na mvua yangu,'Nana Owiti amsifia King Kaka anaposheherekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Nyuma ya kila mwanamume amefanikiwa kuna mwanamke, ni swali au msemo ambao Nana Owiti mkewe King Kaka aliusema
  • Wanandoa Nana Owiti na rappa King Kaka ni miongoni mwa wanandoa mashuhuri ambao hawajakuwa wakitafuta kiki kutoka kwa mashabiki
king kaka-2
king kaka-2

Nyuma ya kila mwanamume amefanikiwa kuna mwanamke, ni swali au msemo ambao Nana Owiti mkewe King Kaka aliusema huku akimwandikia mumewe ujumbe wa kipekee siku yake ya kuzaliwa.

Wanandoa Nana Owiti na rappa King Kaka ni miongoni mwa wanandoa mashuhuri ambao hawajakuwa wakitafuta kiki kutoka kwa mashabiki au kuwa na drama nyingi kama baadhi ya wanandoa mashuhuri.

Huku Kaka akisheherekea siku yake ya kuzaliwa Nana alimwandikia ujumbe wa kipekee, huku akimwambia kwamba ni rafiki wake wa milele.

90226946_2651278888481699_8770703791842362787_n (1)
90226946_2651278888481699_8770703791842362787_n (1)
 

Pia alimsifia jinsi amekuwa akimuunga mkono katika kutimiza ndoto za maisha yake.

"Nyuma ya kila mwanamume __ ??? Kweli, Alinipeleka kazini jana, ameniacha nifanye kazi kila siku mwezi uliopita

Sina mabishano kwamba nina rafiki wa milele. Tunapigana, tunaunda, tunacheka lakini juu ya yote tunajifunza na kufanya vizuri zaidi

Unajua kasoro zangu, haikuweza kuficha uvunjifu wangu, unajua udhaifu wangu lakini bado unaniona nimeshangaza kabisa Siku ya kuzaliwa yenye furaha sana kwa mfumo wangu mkubwa wa msaada..

Wewe ni jua langu na mvua yangu .. Kimsingi unanifanya niwe moto 😂 😂 Niko nawe sambamba kila wakati na kihalisi !!! Heri ya Kuzaliwa," Aliandika Nana.