'Mpe mama pesa aanze biashara' Wakenya wamsuta Dr Kingori

Dr Kingori
Dr Kingori

Mtangazaji wa runinga ya NTV, Dr. Kingori aijipatana taabani na wakenya wakati alipochapisha picha ya mwanamke aliyemshika mkono wakti hakuwa na chochote.

Alipochapisha picha hiyo, Kingori aliwaomba wakenya wampe kazi za kufua na za usafi ili ajikimu kimaisha.

Hata hivyo, ujumbe huo uliwakasirisha wakenya wengi kwani hakuelewa mbona mtangazaji aliye na kazi nzuri asimpe fedha za kujisimamia au za kuanzisha biashara, ilhali anawaomba wakenya kumpa ajira ndogo ndogo.

Kingori aliandika;

Karibu miaka 11 iliyopita, wakati wa wakati wangu wa chini kabisa maishani, bibi huyu hapa, Tiso, alinipa mahali pa kukaa.

Kwa zaidi ya miezi 6, alikuwa mkarimu sana, hakuwahi lalamika na pia alikuwa mmoja wa waliokuwa na imani na kile ninachofanya. (Ni hadithi refu, nitawapea kwa undani hivi karibuni).

Ni mmoja ya watu wenye bidii sana, mtu roho safi na mtu atakaye kuambiwa kilicho moyoni mwake moja kwa moja. Mambo bado hayajamfungukia vile inafaa lakini labda unaweza pia kunisaidia kuwa Baraka katika maisha yake. Patieni Tiso kazi za kusafisha, Kufua na kazi yoyote inayohusiana na kazi za nyumbani.

Unaweza kumfikia kwa: 0741174842 Huyu madam ni ushuhuda kwamba kuna watu wazuri katika ulimwengu huu. Hii dunia yetu ya saa hii kupata mtu anakam kupitia kwako na hata yeye hana! Uliskia wapi? MUNGU ambariki, na wewe kwa njia yoyote ili uweze kuwa baraka katika maisha yake pia. Yeye si mtu wa hand outs, muitie tu job.

Mcheshi DJ Shiti alikuwa miongoni mwa waliomuomba Kingori kumsaidia kujikimu kimaisha.

Aliandika;

Kingori patia huyo Madam 420k anzishe bizz bwana wacha mchezo na #NationMediaGroug Inakulipa 880k per month??? Uko na prado mbili na matatu??? Cheza kama wewe bro nakuaminia or basi uwache akae free kwa ploti zako za pipeline ama kyamaiko???? Please bro do something.... Or umpatie kazi kwa chicken Inn zako Utawala or Ruaka... Do something King's.. 😢😢Please.

Soma baadhi ya jumbe kutoka kwa mashabiki wa Kingori;

Niite jb: You should just give this mum 100k anzishe biashara

Generally: You should be helping her on how to start something for her like business Sasa kufua until when at her age brother fear God oo

Kiki Mbithi: So after hosting you all you can do ni kuuliza watu wako na kazi ya kufua enyewe people forget