'Sijawahi patana na mwanamke huyo,' Msanii B Classic ajibu madai ya ujauzito

Muhtasari
  • Msanii B Classic ajibu madai ya ujauzito
  • Jumatatu Kapoor aliomba msaada wa kumtafuta msanii huyo, baada ya kutoroka, huku akijibu madai hayo alisema kwamba hajui wala hajawahi patana na mwanamke huyo

Msanii chipukizi kutoka Taita Taveta B Classic amejibu madai ya kuweka mwanamke ujauzito na kukataa kujukumikia ujauzito huo kama alivyodai Video Vixen Kapoor.

Jumatatu Kapoor aliomba msaada wa kumtafuta msanii huyo, baada ya kutoroka, huku akijibu madai hayo alisema kwamba hajui wala hajawahi patana na mwanamke huyo.

"Umakini wangu umevutiwa na video inayosambaa mitandaoni iliyo na madai ya uwongo yenye lengo la kuharibu jina langu zuri.

Sijawahi kukutana na mwanamke huyo kwenye video maarufu Kapoor, madai yaliyotolewa humo ni uzushi na uwongo wa mawazo ya watunga.

Tuhuma mbaya na za uwongo juu ya jina langu na tabia yangu haikubaliki kwangu na kampuni za Media ambazo zimeniamini sana.

Hiyo ndiyo yote ningependa kusema," Aliandika B Classic.

Je sababu ya mwanamke huyo kusema madai hayo ni ipi?