Malkia wa Mugithi’ amfichua mpenzi wake kwa mashabiki.

Joyce wa Mamaa aliwahi shukiwa kuhusika kimapenzi na Samidoh

Muhtasari

•Ameonekana kuchapisha picha zilizoandamana na maelezo ya kimapenzi

•Ana mtoto na mtangazaji tajika wa redio

Joyce Wa Mamaa na mpenziwe
Joyce Wa Mamaa na mpenziwe
Image: Facebook

Ni wazi kuwa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Kikuyu Joyce Wa Mamaa amepata jiko baada yake kuonekena akichapisha picha zake na  mwanaume aliyemficha sura kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mwanadada yule aliyekubalika kuwa ‘malkia wa mugithi’ wa sasa kutokana na mtindo wa mziki wake amekuwa akianika picha hizo na kuweka maelezo yaliyopambwa na lugha ya mapenzi mara kwa mara.

“Kwa wenye wamekuwa wakifuatilia hii safari yangu ya mapenzi, tumefika kwa mlima pumzikeni sasa,’ Joyce alichapisha kuwahakikishia mashabiki wake.

Joyce na mchumba wake aliyemficha sura
Joyce na mchumba wake aliyemficha sura
Image: Facebook

Joyce ingawaje hajakubali kuiweka wazi sura ya ashiki yule akionekana kuuficha na emoji kila mara kana kwamba mnalo jambo analoficha.

Wa Mamaa amehusishwa na drama mingi za kimapenzi tangu aanze usanii wake. Aliwahi kuwa  kwa ndoa na mtangazaji tajika wa redio ya Kikuyu anayejulikana kama Munyeki Sonko the second ila haikufaulu. Wawili hao walifanikiwa kuwa na mtoto mmoja ambaye anaishi na Joyce.

Joyce alishukiwa kuwa na mahusiano na nyota wa muziki wa Mugithi almurufu kama Samidoh. Wawili hao walichochea gumzo moto mtandaoni baada ya picha na video zenye utata kuenea mtandaoni wakati walipokuwa wameenda Dubai pamoja kwa shughuli ya kimuziki.

Wanamziki hao wawili waliachilia kibao kilichojulikana kama “Wendo wi cama”(Mapenzi matamu) ambacho kilivuma sana nchini.

Inaaminika kuwa mwanadada yule pia liwahi kuwa na mahusiano na mwanamziki John Njagi, madai ambayo ameyakanusha mara kadhaa kwenye mahojiano mbalimbali. Bwana Njagi aliwahi fanya kazi ya kimuziki pamoja na Joyce hapo awali.