logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilimpata mpenzi wangu na mwanamke aliyekomaa kitandani mchana peupe-Mwanamke asimulia

Lakini sababu ya mwanake huyo kusema amekata tamaa kwa wanaume ni ipi?

image
na Radio Jambo

Habari15 May 2021 - 12:15

Muhtasari


  • Nilimpata mpenzi wangu na mwanamke aliyekomaa kitandani mchana peupe
black-woman-crying-

 Karne hii ya sasa jinsia zote mbili za kizazi hiki cha sasa hawataki majukumu, katika maisha yao kwani kila mmoja anapenda maisha yake au tuseme wanapenda pesa sana.

Nikifanya ziara zangu nilipatana na mwanamke mmoja ambaye alikuwa amevunjika moyoni, huku akiwa na huzuni mwingi.

Lakini sababu ya mwanake huyo kusema amekata tamaa kwa wanaume ni ipi?

 

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa na mchumba wa miaka 3, wazazi wake walinifahamu na wangu walimfahamu sana kwa maana tulikuwa tumeagana kwamba tutafunga ndoa mwaka wa 2022

Mapema mwaka huu alibadili tabia na hata alikuwa ananiambia nisijaribu kumpigia simu usiku bali hakuniambia sababu 

Nilimpa muda lakini nilisikia funu u kwamba amechukuliwa au tusema ameolewa na mwanamke ambaye amekomaa

Niliamua kuenda kwake bila ya kumwambia na niliwapata akiwa na mwanamke huyo kitandani na nyumbani kwake wakifanya mapenzi mchana peupe

Naskia tu nimechoka na mapenzi ya sasa wacha nikae jinsi nilivyo," Alieleza mwanamke huyo.

Wakati huu vijana wenye umri mdogo wamechukuliwa na akina mama na wasichana nao wamechukuliwa na wazee, huku wengi wakipoteza mwelekeo wa maisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved