Khaligraph Jones awasaidia wakazi wa Kayole na vyakula

Muhtasari
  • Msanii na Rappa wa humu nchini Kaligraph Jones siku ya Jumamosi Mei 15, alipeleka msaada wa chakula katika eneo la Kayole kaunti ya Nairobi
  • Haya yanajiri wiki chache baada ya msanii huyo kukutana na naibu rais William Ruto na kumpa vilio vya wasanii na vile wanateseka
  • Wakati huu wa janga la corona wengi wa wananchi wamepoteza makazi yao na hata wengi kupitta wakati mgumu
khali-e1471415170725
khali-e1471415170725

Msanii na Rappa wa humu nchini Kaligraph Jones siku ya JUmamosi Mei 15, alipeleka msaada wa chakula katika eneo la Kayole kaunti ya Nairobi.

Haya yanajiri wiki chache baada ya msanii huyo kukutana na naibu rais William Ruto na kumpa vilio vya wasanii na vile wanateseka.

Wakati huu wa janga la corona wengi wa wananchi wamepoteza makazi yao na hata wengi kupitta wakati mgumu.

 

Kupitia kwenye uurasa wake wa instagram msanii huyo alipakia picha huku akiwa amesimama na watoto tayari kusambaza chakula.

Pia kwenye mitanda hiyo hiyo alipakia video huku watu wakipokea unga.

Huu hapa ujumbe wake rappa huyo;

"Leo Ilikuwa Siku Njema, tuliweza Kutoa Kitu Kidogo Kwa watu wasiojiweza wakati wa nyakati hizi ngumu za Corona. Asantenyote  kwa kuheshimu OG .." Aliandika JOnes

Msanii huyo alilelewa mtaa wa Kayole hivyo basi aliwasaidia watu wa mtaa wake kuwahakikishia kwamba hajawasahau hasa wwakati huu mgumu.

Hizi hapa jumbe za maashabiki;

njoroshirandula: God bless you

 

riyamaally: Kila la kheri ubarikiwe zaidi MUNGU Akujalie JAZA ya ziada apaongeze Ulipopunguza Amin 🙏🤲@khaligraph_jones

captain_pasil: 👏👏👏👏👏 respect to the Og

msaniibabji: Leading by example 🔥🔥🔥🔥🔥🔥❤️Og