Mimi ndiye mama pekee ambaye huwapa watoto wake pombe-Akothee

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alipakia video ya mwanawe Rue Baby akibugia vileo
  • Katika video hiyo anasikika akimwambia Rue kwamba anamfanana baba yake
  • Baada ya kupakia video hiyo aliandika ujumbe na kusema kwamba yeye ndiye mama ambaye huwapa wanawe pombe
rue baby
rue baby

Msanii Akothee atafanya lolote au chochote ili kuwalinda wanawe,hasa wasichana wake kutokana na wanaume wanaouzoefu wa kuwatumia wanawake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alipakia video ya mwanawe Rue Baby akibugia vileo.

Katika video hiyo anasikika akimwambia Rue kwamba anamfanana baba yake.

 

Baada ya kupakia video hiyo aliandika ujumbe na kusema kwamba yeye ndiye mama ambaye huwapa wanawe pombe.

Pia alimshauri mwanawe abugia atalipa kama mama na wala sio mwanamume ambaye atalipa na kumtumia mwanawe vibaya.

"Mimi ndiye mama pekee ambaye huwapa watoto wake pombe,kunywa wakati nakuona kuliko kunywa wwakati sikuoni

Kunywa nitalipa gharama kuliko mtu mwingine akulipie na kisha akuharibie maisha yako,milele kwa ajili ya usiku mmoja,"Aliandika Akothee.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya ujumbe wake Akothee;

rue.baby: Why did you have to spoil the moment though

miriamokello: jared en ng'a yawa? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚the way she has folded her face(amekunja sura)

dianfah_ke: Eeeeish.....Madam Boss mwenyewe ❀️❀️

sanyatiwa7: Mbona Hilo jina Jared imemchoke hivoπŸ˜‚

nyamagwa.victoria: Sasa who is Jared πŸ˜‚ tunataka kumwona we compare