logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Niachwe Jamani!Wema Sepetu akomesha ugomvi wake na Zari Hassan

Pia muigizaji huyo alisema aachwe kwani hataki drama na mtu yeyote.

image
na Radio Jambo

Burudani16 May 2021 - 06:40

Muhtasari


  • Wema Sepetu akomesha ugomvi wake na Zari Hassan, huku akisema anapawa kuachwa kwani hataki drama
wema 5 (1)

Mpea Wiki jana waliokuwa wapenzi wa staa wa bongo Diamond Platnumz, Zari Hassan na Wema Sepetu walishambuliana kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja akimtupia maneno makali mwenzake.

Wema alikuwa mpenzi wake wa Diamond wa kwanza kufahamika na mashabiki, huku wakiachana baada ya muda mfupi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram wa Wema alisema kwamba huwwa ananyamaza kwa maana kila mtu huona kwamba ndiye mwenye makosa katika kila ugomvi.

 

Pia muigizaji huyo alisema aachwe kwani hataki drama na mtu yeyote.

"Naomba niseme hivi, Sipendi chokochoko... Maana Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha sio...

Kama maneno always yanaanziaga upande wa pili but ilivyo ada Wema ndo huonekana mwenye tatizo... Nimechoka... Cause mi mdomo mchafu ninao haswaaaa but kuamuaga kukaa kimya nisionekane mjinga basi...

Its Eid at the end of the day... Sitaki chokochoko...‼️ Ifike point niachwe jamani," Alisema WEma.

Je ugomvi wa wawili hao utaendeela mpaka lini licha ya muigizaji Wema kukomesha ugomvi huo, na kiini cha ugomvi huo ni nini.

Ni maswali ambayo wanamitandao wamebaki nayo akilini mwao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved