Nimewasamehe wale walinitusi,'Msanii Justina Syokau awaambia mashabiki

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau amekuwa akivuma kwenye mitandao ya kijamii kwa muda sasa baada ya kufichua kwamba anahitaji msaada wa pesa kutoka kwa wakenya

Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau amekuwa akivuma kwenye mitandao ya kijamii kwa muda sasa baada ya kufichua kwamba anahitaji msaada wa pesa kutoka kwa wakenya.

Siku ya JUmatatu kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alipakia video na kusema kwamba amewasamehe wale wote walimtusi alipokuwa anapitia magumu.

PIa aliwashauri na kuwaonya mashabiki kwaba sio vyema kwa mtu kumtusi au kuongea mambaya kuhusu mtu akiwa mgonjwa kwani hawajui wala kufahamu kile wanapitia wakati huo.

Baadhi ya wanamitandao walimkejeli msanii huyo na kumwamboa kwamba anapaswa kuuza mali yake aliyonayo ili apate pesa na awache kuwatapeli wakenya.

KUpitia kwenye video iyo, msanii Syokau alidai kwamba amebakisha deni ya milioni 6.7, huku mashabiki wakizua mjadla mkali kwenye mitandao hiyo.

Pia aliwashukuru mashabiki wake na wale wote ambao wamemshika mkono na kumsaidia,alisema kuwa na ploti lakini hawezi uza kwa bei ya chini kwa maana anahitaji msaada.

"Bwana asifiwe, Mungu awabariki kwa kunishika mkono, asanteni kwa maombi yenu, nimeona watu wakisema na kutoa maoni kwamba natapeli watu

Kuna wale wanasema nifariki,lakini siwezi kufa kwa sasawale wote walinitusi nataka kuwaambia kwamba nimewasamehe

Kama mtu ni mgonjwa na humpendi haya basi usijaribu kumwamndikia matusi kwa maana hujui nini wanapitia, kama hunipendi usiandike kitu mbaya ama wacha kuwa shabiki yangu," Alisema Syokau.

Hii hapa video ya usemi wake;