'Kazi ya Mungu haina makosa,'Willy Paul azungumza baada ya kumsajili mwanamuziki mpya

Muhtasari
  • Willy Paul azungumza baada ya kumsajili mwanamuziki mpya
  • Msanii huyo amemsajili manii mpya kwenye lebo yake ya muziki huku akiwasihi wakenya wamshike mkono
  • Pia aliahahidi mwaka huu atarekebisha kile chote kiliharibiwa katika tasnia ya burudani kwa miaka mingi
Willy Paul
Willy Paul

Msanii Willy Paul amezidi kutia bidii kila kuchao na hata kukuza talanta za wanamuziki chipukizi.

Mapema mwaka huu alimsajili msanii wa kike Miss P kwenye lebo yake ya muziki na amekuwa akitoa collabo naye na kufanya kazi vyema.

Paul anajulikana na mashabiki wake tangu aanze safari yake ya usanii.

Msanii huyo amemsajili manii mpya kwenye lebo yake ya muziki huku akiwasihi wakenya wamshike mkono.

Pia aliahahidi mwaka huu atarekebisha kile chote kiliharibiwa katika tasnia ya burudani kwa miaka mingi.

Paul alidai kwamba kenya kuna talanta nyingi ambazo zinahitaji kukuzwa,na kuwa wakati umefika wasanii waonyeshe ulimwengi kile wanaweza kufanya.

"Habari za asubuhi familia, tumaini uko tayari kwa huyu! Wakitoa tunatoa! Kenya ina talanta nyingi sana, tafadhali tuunge mkono yetu wenyewe

Fuata msanii wangu wa Kiume aliyesainiwa hivi karibuni @klons_kenya sasa kwa zaidi. Ahadi yangu mwaka huu ni kurekebisha sehemu zilizoharibiwa za tasnia yetu

Watu hapa nje ni wabinafsi sana, wanajiona sana kusaidia wale wanaohitaji. Tulianza na @misspicasah sasa tuko hapa na talanta nyingine mpya @klons_kenya

Na @saldido_international haisimami kwa chochote ... naamini ni wakati wake kuonyesha ulimwengu kile tunaweza kufanya kweli !! Kazi ya Mungu haina Makosa ..

Jambo lingine, kurudisha hakukugharimu chochote! Kumbuka, maudhui mazuri na safi ndio watu wanataka kweli!" Alisema Willy.