Je msanii Nyota Ndogo amejifunza somo baada ya mumewe kumnyamazia?

Muhtasari
  • Je msanii NYota amejifunza nini kutokana na drama yake?
  • Huku akiwa kwenye mahojiano Nyota alidai kwamba ataenda Denmark kumtafuta mumewe baada ya kunyamazia kwa muda
  • Baadhi ya wanamitandao walimwambia kwamba mumewe alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n

Ndoa ya msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo ilisambaratika baada ya tarehe 1 Aprili 2021, hii ni baada ya msanii uyo kumtania mumewe kwamba ana ujauzito.

Huku akiwa kwenye mahojiano Nyota alidai kwamba ataenda Denmark kumtafuta mumewe baada ya kunyamazia kwa muda.

Baadhi ya wanamitandao walimwambia kwamba mumewe alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha.

"Nimekuwa nikizungumza na mwanawe, lakini mwanawe akimwambia kuhusu jina langu anakata simu

Amenipa block kila mahali, napanga kuenda DEnmark ilitusuhishe mambo pamoja akinifukuza ni sawa pia

Sikubaliana na maoni ya mashabiki kwamba alikuwa anatafuta sababu ya kuniacha, kwa maana amenijengea nyumbani saba na hawezi kuniacha," Alisema Nyota akiwa kwe ye mahojiano.

Je msanii huyo amejifunza yapi, baada ya drama yake, kwana kile nyota amejifunza ni kwamba kutaniana sio vyema kwanza kwa jambo lile mlizungumzia awali.

Pia kama wapenzi  sio kila kitu cha kutaniana, kwani hujui mwenzako anapitia nini katika mawazo yake na kile anahitaji kwa wakati huo.

Mbali na mumewe Nyota pia amekuwa akijifunza kwamba ni vyema kupigania mapenzi yake licha ya kejeli ambazo unapokea kutoka kwa marafiki na wanamitandao.

Msanii huyo pia anaweza kuwa amejifunza kwamba pesa sio kila kitu kwani unahitaji mapenzi ya mwenzio, na vyema kuheshimu mipaka ya mwenzako katika maisha yake.

Pia kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrama msanii huyo aligadhabishwa na wanawake ambao wamekuwa wakimtumia mumewe jumbe, huku akiwashauri wangoje apewe talaka kama atapewa.