Mcheshi Jemutai afichua alimsamehe mchekeshaji Hamo

Muhtasari
  • Jemutai akiri kumsamehe Professor Hamo
  • Haya yalijiri baada ya Jemutai kufichua kuwa Hamo hajakuwa akijukumikia mahitaji ya wanawe.
jemutaionstage
jemutaionstage

Baada ya ripoti ya DNA kutokea na kuonyesha kwamba mchekeshaji wa kipindi cha churchill  Professor Hamo ni baba yake watoto wa mcheshi Jemutai aliomba msamaha.

Haya yalijiri baada ya Jemutai kufichua kuwa Hamo hajakuwa akijukumikia mahitaji ya wanawe.

Hamo kupitia kwenye ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa instagram aliomba wanawe,familia na mashabiki msamaha kwa yale yote yalitokea.

"Nawapenda wote na nitahakikisha nipo hapa kwa ajili yenu 🥰. Familia ya RMS poleni kwa kuburuzwa katika haya yote unajua walikuwa hapa wiki 3 mapema

Na kwenu mashabiki wangu. Bila wewe mimi ni Herman tu. Pamoja na wewe mimi ni Prof Hamo

Niruhusu niongeze sura nyingine katika "Kitabu Changu Cha .." Samahani sana kwa kukuangusha

Bado sipo lakini ninafanya kazi kwa kuwa mtu anayewajibika, baba, mume na mtu. Mungu ni Mwema .. !!!,"

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram mmoja wa mashabiki wake Jemutai alimuuliza kama alimsamehe Hamo na akasema kwamba alimsamehe.

Je ulimsamehe professor Hamo?" Aliuliza shabiki.

"Ndio," Alijibu Jemutai.

Pia mcheshi huyo alisema kwamba hayuko tayari kumpata mtoto mwingine.