'Ni dhahiri ana shida,'Mwanasiasa Alinur ajitolea kumsaidia msanii Embarambamba

Muhtasari
  • Mwanasiasa Honalinur ajitolea kumsaidia msanii Embarambamba
  • Ni tabia ya wakenya na wanamitandao kumuhukumu mtu bila ya kujua kile anachopitia na sababu ya kufanya jambo fulani

Habari njema kwa msanii Embarambamba na mashabiki wake baada ya mwanasiasa Honalinur kujitolea kumsaidia kwa ajili ya kazi yake.

Ni tabia ya wakenya na wanamitandao kumuhukumu mtu bila ya kujua kile anachopitia na sababu ya kufanya jambo fulani.

Msanii Embarambamba ambaye anavuma sana kwenye mitandao ya kijamii, amekuwa akipokea kejeli nyingi sana huku baadhi ya wanamitandao wakidai kwamba hana akili timamu.

Licha ya wakenya wengi kumkejeli Embarambamba baada ya video yake akisakata densi, mwanasiasa huyo amemtetea na kusema atamsaidia.

"Tofauti na watu wengi sitaenda kuketi kiti cha nyuma na kulaani Embarambamba bila kumpa msaada wowote.

Ni dhahiri ana shida. Sasa kazi yake imekufa nusu. Anahitaji msaada haraka au tutapoteza talanta hii adimu. Nitamtafuta na kumsaidia mara moja," Alise,ma Honalinur.