FAMILIA YA WAJESUS

''Si mwanaume wa kawaida, ni mfalme" Milly amsifu Kabi

Wanandoa Kabi na Milly Wajesus waendelea kushangaza wengi na mapenzi kati yao licha ya changamoto zilizokumba ndoa yao hivi majuzi

Muhtasari

“Nakupenda sana malaika. Bila wewe mimi ni mvulana mdogo tu na paji la uso kubwa na nywele kwa mguu, unanikamilisha” Kabi alimuandikia Milly.

Kabi na Milly Wajesus
Kabi na Milly Wajesus
Image: Instagram

Wanandoa Peter Kabi (Kabi Wajesus)  na Millicent Wambui(Milly Wajesus) wameendelea kuwashangaza wengi kutokana na mapenzi wanayoonyesha mitandaoni licha ya masaibu yaliyokumba ndoa yao wiki chache zilizopita.

Siku ya Jumatatu, Milly alimsherehekea mumuwe kwa ujumbe wa kusisimua huku akimsifia kuwa anayependa sana, mcha Mungu na mwenye bidii sana.

“Si mwanaume wa kawaida, yeye ni mfalme. Ni mtu anapenda kuomba, anajua kupenda na mwenye bidii sana. Najivunia sana kumuita mume wangu." Milly aliandika huku akimuarifu mumewe.

Kwa upande wake Kabi, alimuambia Milly kuwa anampenda sana na anamkamilisha kama mwanaume.

“Nakupenda sana malaika. Bila wewe mimi ni mvulana mdogo tu na paji la uso kubwa na nywele kwa mguu, unanikamilisha” Kabi alimjibu Milly.

ujumbe wa Kabi
ujumbe wa Kabi

Wengi mitandaoni walimsuta sana Kabi kwa kukiri kuwa ana mtoto na binamu yake huku wengine wakikadiria kuwa huo ni mwisho wa ndoa ya wawili hao. Hata hivyo, wapenzi hao wameendelea kuthibitishia makosa wanaowatilia shaka.