Mheshimu mwanamume anayeweza kuponya moyo ambao hakuvunja-Betty Bayo

Muhtasari
  • Betty Bayo amtambulisha mpenzi wake
Betty Bayo

Msanii wa nyimbo za injili Betty Bayo amemtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki  mika chache baada ya kuachana na mumewe Pasta Kanyari.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia picha ya mwanamume huku akiwashauri mashabiki wanapaswa kuheshimu mwanamume ambaye anaweza kuponya moyo ambao hakuuvunja.

Huku akimalizia ujumbe wake alisema kwamba ni yesu tu anaweza fanya hayo, pamoja na kutunza watoto ambao sio wake.

"Mheshimu mwanamume anayeweza kuponya moyo ambao hakuvunja na kumlea mtoto ambaye sio wakea.😘😘😘ni Yesu tu anayeweza kufanya hivyo," Aliandika Betty.

Mwaka jana Betty alipakia picha ya mwanamumme akiwa anavisha pete ya uchumba ambapo Kanyari hakupendezwa na kitendo hicho.

KUlingana na mashabiki na wanamitandao msanii huyo amepata mpenzi.