MNIKOME!

Nyota Ndogo akashifu wanaosema ni pesa tu anataka

"Mna ushenzi sana roho zenu za korosho kuchomwa!" Nyota ndogo awasuta wanaokejeli hali yake

Muhtasari

• Nyota Ndogo amekasirishwa sana na madai kuwa ni pesa za mpenzi wake mzungu tu anataka ila si mapenzi.

•Alikiri kuachwa na mpenziwe mwezini Aprili amekuwa akichapisha jumbe za kumwagiza mumewe kumrudia kwenye mtandao wa Instagram huku akidai kuwa amefungiwa namna yote anayoweza kumfikia nayo.

Nyota Ndogo na mumewe
Nyota Ndogo na mumewe
Image: Instagram

Mwanamuziki Nyota Ndogo ameonekana kukasirishwa sana na madai kuwa ni pesa za mpenzi wake mzungu tu anataka ila si mapenzi.

Msanii huyo toka Pwani amewasuta wale ambao wamekuwa wakikejeli hali yake huku akiwaarifu kuwa hana haja na pesa za wenyewe kwani anajua kujitafutia.

"Hee Wakenya jamani mimi nimeshachoka kusema najua kusaka pesa zangu kwa njia iliyo sawa ila uvivu wenu umefanya mnaona kila mtu mvivu. Lakini nani hapendi hela? Mna ushenzi sana roho zenu za korosho kuchomwa. Mnatamani kila mtu awaombe ili mumseme. Haya,nataka hizo za Mungui mimi simushukuru siwaombi jamani!" Nyota Ndogo aliandika huku akizungumziwa ripoti iliyodai kuwa analilia pesa tu.

Nyota Ndogo ambaye alikiri kuachwa na mpenziwe mwezini Aprili amekuwa akichapisha jumbe za kumwagiza mumewe kumrudia kwenye mtandao wa Instagram huku akidai kuwa amefungiwa namna yote anayoweza kumfikia nayo.