Ghost Mulee arejea kazini awashukuru mashabiki kwa kumuombea

Muhtasari
  • Ghost Mulee arejea kazini awashukuru mashabiki kwa kumuombea
Ghost Mulee

Mtangazaji wa radiojambo Jacob Ghost Mulee, ilikuwa siku ya kwanza Alhamisi kuingiza studioni baada ya kuwa India na kukwama nchini humo kwa miezi miwili.

Mashabiki wake walimpeza, huku wengi wakisema kwamba walipeza kicheko chake.

Haya basi msitie shaka wala kuwa na wasiwasi kwani mtangazaji huyo amerejea kazini, baada ya kupokea matibabu.

Kupitia kwenye video, iliyopakiwa kwenye ukurasa wa facebook wa radiojambo, mtangazaji huyo aliwashukuru mashabiki kwa maombi yao, na kuwaarifu ya kwamba amerejea.

"Shukrani nyingi kwa wale waliniombea nilipokuwa Delhi, unajua india ilikuwa katika lockdown, nilikuwa naskikiza kipindi cha Gidi na Ghost nilipokuwa India

Pia nilikuwa nasikiza kipindi cha bustani la Massawe, usingalie ndevu zangu huko Delhi vinyozi vilikuwa vimegungwa." Alisema Ghost.

Ghost Mulee amerejea baada ya kukwama India kwa miezi 2 kufuatia marufuku ya usafiri wa ndege kutoka nchini humo kuingia Kenya. Karibu sana Ghost. Tulikuwa tumekupezaaaa😍😍 #GidiNaGhostAsubuhi #OngeaUsikike

Posted by Radio Jambo on Thursday, May 27, 2021

Huku akimtania kinyozi wake alisema kwamba.

"Kinyozi wangu ameniambia atanilipisha miezi miwili, unanyoa ndevu au miezi," Ghost alimtania.