Orodha ya wanasiasa waliohudhuria harusi ya mwanawe DP Ruto

Muhtasari
  • Orodha ya wanasiasa waliohudhuria harusi ya mwanawe DP Ruto
Image: Hisani

Alhamisi ilikuwa siku kuu kwa naibu rais William Ruto, kwani mwanawe alikuwa anafunga harusi na mpenzi wake.

Jamaa,familia,marafiki,wanasaisa, watu mashuhuri na walioalikwa walihudhuria hafla hiyo ya kutamausha.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wandani wa DP haswa kwenye kambi ya Tangatanga huku wenzao wa Kieleweke wakichungulia tu kwa umbali.

Rais Uhuru Kenyatta, Mama Margret Kenyetta au jamaa wa familia yao hawakuonekana kwenye sherehe hiyo.

Hii hapa orodha ya wanasiasa ambao walihudhuria hafla hiyo;

1.Musalia Mudavadi

KInara wa chama cha ANC alielea tofauti zake za kisiasa na kuhudhuria sheherehe hiyo, ambayo ilikuwa ni ya kifani.

Musalia Mudvadi alionekana mchangamfu na mwenye furaha.

2.Isaac Mwaura 

Baada ya mwanasiasa huyo kutimuliwa JUbilee kwa madai ya ukaidi  ilikuwa mara yake ya kwanza kujitokeza kwa umma.

Ni furaha ya kila mzazi kumuona mwanawe akiwa na furaha na kuvuka upande mwingine wa maisha.

Kwake June ilikuwa ndoto ya maisha ambayo ilitimia Mei 27.