'Upendo wa Kweli Unajaribiwa katika nyakati ngumu zaidi,'Bahati asema

Muhtasari
  • Mashabiki wazua gumzo mitandaoni baada ya ujumbe wake Bahati
  • Mashabiki na wanamitandao wanamfahamu msanii Bahati kama anayependa kutafuta kiki kwa vyovyote

Mashabiki na wanamitandao wanamfahamu msanii Bahati kama anayependa kutafuta kiki kwa vyovyote.

Wanamitandao walishindwa kama msanii huyo anatafuta kii kutokana na ujumbe wake wa awali kuwa atachukua mapumziko kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Huku akiwatangazia mashabiki wake habari hizo, alisema kwamba amekuwa akijitolea kwa watu wengi sana na kuwatakia mafanikio maishani mwao bali huwa ana baki na swali moja tu.

Kama watu hao hunena baraka na kumtakia mafanikio maishani mwake.

Pia Bahati aliguzia upendo, na kuwauliza mashabiki wake kama wanafahamu upendo wa kweli ni upi, na kuwa huwa unajaribiwa katika nyakati ngumu zaidi.

Nitachukua muda nitoke kwe ye mitandao ya kijamii Kutafakari tu Maisha Yangu: Lakini ningependa Kukuacha na Kitu cha Kutafakari ... Upendo na Mauti!

Je! Umewahi kujiuliza Upendo wa Kweli ni nini! Je! Ipo na Je! Mtu ambaye Anakuambia kila wakati "NAKUPENDA" anamaanisha ???

Upendo wa Kweli Unajaribiwa katika nyakati ngumu zaidi; lakini Je! Upendo bado umeonyeshwa kwako na Watu unaowapenda katika Nyakati zako ngumu zaidi ???

Ninaishi Maisha ya Kujitolea kwa Watu, Kusaidia Ndoto na Maono ya Watu Ninaowapenda. Ninapenda Kuona Watu Ninaowapenda Wamefanikiwa lakini kwa Nyakati Nimeachwa nikifikiria kama Wangetamani Sawa Kwangu ... ikiwa Wanaweza Kutoa Dhabihu kwa ajili Yangu ... Kufikiria tu!" Aliandika Bahati.

Bahati alishindwa ni kwa muda upi, anayekupenda atakuomboleza andapo umefariki.

"Daima ni ngumu kufikiria juu ya hili lakini ikiwa Mungu Anaamua Utakufa leo; Je! Mtu Unayempenda Atakuombolezea Kwa Muda Gani ... Atakulilia au watakubadilisha Mara Moja Upendo Wako kwa Mtu Mwingine !!!"