Mimi siwaogopi Watanzania na matusi yao-Akothee aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Siku chache baada ya mwanabiashara na msanii tokea kenya Akothee aliwakashifu na kuwasuta Watanzania baada ya kudai kwamba haikuwa vyema kwao, Akothee kushinda Diamond kwa utajiri
  • Hii ni baada ya Forbes kutoa orodha wasanii tajiri Afrika
  • Wiki iliyopita staa wa bongo, Diamond Platnumz alisuta kampuni ya Forbes baada ya kumweka kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika
Akothee
Akothee
Image: Hisani: Instagram

Siku chache baada ya mwanabiashara na msanii tokea kenya Akothee aliwakashifu na kuwasuta Watanzania baada ya kudai kwamba haikuwa vyema kwao, Akothee kushinda Diamond kwa utajiri.

Hii ni baada ya Forbes kutoa orodha wasanii tajiri Afrika.

Wiki iliyopita staa wa bongo, Diamond Platnumz alisuta kampuni ya Forbes baada ya kumweka kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Mwanamuziki huyo tokea Tanzania aliwasihi Forbes kufanya utafiti dhabiti kabla ya kuweka jina lake kwenye orodha ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothe ameeka wazi kwamba hawaogopi watanzania kwa matusi yao, kwani amewashinda kwa vingi.

"Mimi siwaogopi watanzania na matusi yao,naweza kuwashinda kwa sentensi tatu tu, kuna tofauti kubwa, kuwa maji,tajiri, na kuwa na mali 

Waambie kwa kiswahili Pesa Zenu hazinihusuKaulizeni forbes watengengeze listi mpya , muwekwe number 1Forbes Sio wuon Oyoo πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£Kwani wale waume wote toka number 1 Hadi 8 hamkuwaonaMbona mwanamke kafanya mupaniki?Ala? Chukueni Number Zote," Aliandika Akothee.