Rapa Noti Flow hatimaye ajitambulisha kuwa shoga

Muhtasari
  • Rapa Noti Flow ameonyesha rasmi kuwa yuko kwenye uhusiano na rafiki wa kike, anayejulikana kama Mfalme Alami

Rapa Noti Flow ameonyesha rasmi kuwa yuko kwenye uhusiano na rafiki wa kike, anayejulikana kama Mfalme Alami.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram, Noti Flow alishiriki tena video na King Alami huku mashabiki wakisifia mapenzi yao, na kuonekana wakiwa kwenye mahabara  ya mapenzi kweli kweli.

Mapema mwezi wa Mei, uhusiano wa rapa huyo na King Alami ulitoa uvumi kwamba walikuwa wakichumbiana kwani wote walionekana wazuri pamoja.

"Usiku wetu wa kwanza kutengana tangu tuhamie pamoja na ninaamka kwa hii 🥺😭😭😭😭 Ananippeda kama vile nampenda 💘 Hakuna mtu anayepaswa kutenganisha  aina hii ya mapenzi ❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️🦄️ 🦄 🌈 ," Aliandika Noti Flow.

KUpitia kwenye picha nyingine aliopakia wakiwa wawili Noti flow aliandika ujumbe  unaodhitibitisha kuwa ni shoga  katika ujumbe huo alisema haya.

"Kila kitu nilichokuwa nikitaka ndani yake nimepata kwake ❤️."

Noti Flow hapo zamani alikuwa kwenye uhusiano na rapa mwenzake Kanali Mustapha lakini wawili hao wakaachana.

Noti Flow kwa upande wake alisimulia kuwa aliamua kutia kikomo kwa uhusiano huo kutokana na Mustafa kukosa kuwa na malengo mwafaka kwa maisha .