'Achana na mabibi zangu,'Eric Omondi amwambia Ringtone, msanii huyo amjibu

Muhtasari
  • Mchekeshaji Eric amsihi Ringtone asifanye haya

Je kipindi cha mchekeshaji Eric Omondi kitarejea? ni swali ambalo wanamitandao wamesalia nalo vichwani mwao baada ya Eric Omondi kusema kwamba anatarajia kuwaleta wanawake warembo nchini.

Hii ni baada ya kumuonya msanii wa nyimbo za injili awachane na wanawake wake, kwani hivi karibuni anawaleta wanawake kutoka Sudan kusini,Rwanda,Nigeria na Ethiopia.

Omondi aliweka wazi wakati huu lazima ampate bibi, na mpenzi wake wa maisha.

"Rais lazima aunge mkono muziki mzuri. Huyu Kijana ako na na wito wa juu na kipawa kutoka juu mbinguni...Shida tu ni awachane na mabibi zangu...niko karibu kuwaleta wanawake warembo nchini kenya kutoka  ETHIOPIA, RWANDA, SUDAN KUSINI na NIGERIA bwana CHAIRMAN tafadhali usiwafagie kwa sababu wakati huu lazima nipate mke. Naomba," Aliandika Eric.

Kw aupande wake msanii Ringtone, alimjibu na kumwambia kwamba hana haja na wanawake wake.

"Ndugu yangu, sina biashara yeyote, ya kuwaiba wake wako," Alimjibu Ringtone.