Jifunze kupona kutoka kwa kuumia kwako-Anerlisa awashauri mashabiki

Muhtasari
  • Mwanabiashara Anerlisa Muigai, alivuma sana kwenye mitandao ya kijamii wiki chache zilizopita baada ya kuachana na mumewe msanii kutoka Tanzania Benpol

Mwanabiashara Anerlisa Muigai, alivuma sana kwenye mitandao ya kijamii wiki chache zilizopita baada ya kuachana na mumewe msanii kutoka Tanzania Benpol.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Anerlisa amewashauri mashabiki wake jinsi ya kujifunza kupona kutokana na maumivu yao ya awali.

Pia aliwashauri hapaswi kulaumu tukio ambalo walipitia katika maisha yao ya sasa.

"Ikiwa unatumia maisha yako yote kwa mawazo ya shida yako ambayo ilikusumbua na ndio sababu  ya jinsi vile ulivyo kwa sasa badala ya kujifunza jinsi ya kuponya na kukua kutoka kwa shida yako, wewe ni tatizo lako mwenyewe," Anerlisa Alisema.

Baada ya kuachana na mumewe Anerlisa alitangaza habari hizo kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram.

"Nataka kuweka mambo wazi kuwa nilisaini chochote kilichohitajika kusainiwa, na sitamani kuhusishwa na mtu yeyote,"