Nadhani wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni wanapaswa kuendelea na elimu-Akothee

Muhtasari
  • Akothee asema wasichana wenye ujauzito wanapaswa kuendelea na masomo
  • Hili linaashiria kwamba masomo ya wasichana wengi hukatizwa kwa ajili ya sababu kama hiyo
  • Lakini wanachosahau wengi ni kuwa ujauzito sio ugonjwa wala virusi
Esther Akoth

Mwanabiashara na msanii Esther Akoth maarufu Akothee amechangia katika mjadala unaoendelea nini kitakachofanyiwa wasichana ambao wanapata ujauzito bado wakiwa shule au wanaoendelea na masomo yao.

Kulingana na mwanamuziki huyo , wasichana wanaoenda shule wanaopata ujauzito hawapaswi kurudishwa nyumbani, na badala yake wanapaswa kuruhusiwa kuendelea na masomo isipokuwa afya yao itathibitisha vinginevyo.

Asilimia kubwa ya wasichana kuacha shule kwa ajili ya ujauzito imeshuhudiwa nchini hasa wakati wa janga la corona wasichana wengi hawakurudi shule zilipofunguliwa kwani walikuwa wajawazito.

Hili linaashiria kwamba masomo ya wasichana wengi hukatizwa kwa ajili ya sababu kama hiyo.

Lakini wanachosahau wengi ni kuwa ujauzito sio ugonjwa wala virusi.

"Na nadhani wasichana wote wanaopata mimba wakiwa shulenihawapaswi kupelekwa nyumbani

Lakini wanapaswa kuruhusiwa kuendelea na elimu isipokuwa afya yao itathibitisha vinginevyo. Mimba sio kufariki, ni usumbufu wa muda unaokuja na baraka kubwa. Unafikiria nini,"Alissema Akothee.