Nimerudi! Msanii Bahati atangaza kutoa albamu mpya

Muhtasari
  • Msanii arejea mitandaoni na habari njema
  • Kulingana na msanii huyo, wasanii  wa humu nchini wanapaswa kuketi kitako na kalamu na kitabu na kunakili yale anaenda kufanya

Siku chache zilizopita msanii Kevin Bahati kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alitangaza kuchukua mapumziko kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Haya basi habari njema kwa mashabiki ni kwamba amerejea, na hajarejea tu bali amerudi na habari njema.

Kulingana na msanii huyo, wasanii  wa humu nchini wanapaswa kuketi kitako na kalamu na kitabu na kunakili yale anaenda kufanya.

Msanii huyo alisema kwamba anaenda kutoa albamu mpya na ya kupigiwa mfano na wengi.

"NIMERUDI!!! nilichukua Mapumziko ya Siku chache Kuruhusu Msanii yeyote Anayetaka Kutoa Wimbo, EP au Albamu ya Kufanya Hivyo! 

Kwa hivyo ikiwa bado haujafanya hivyo Wakati umekwisha! Pumzika ... Siku 90 Zifuatazo Zitakuwa Zangu!

Ndio wakati wa albamu yangu ya kuweka miaka yangu7 kwenye tasnia ya muziki !!! Sijui Kuweka haya au kusema ili bado niwe mnyanyekevu Waambie Wanamuziki wenzako wapumzike tu, Kaa chini Chukua Kitabu cha Kumbuka niko karibu kuwafundisha Jinsi ya kutengeneza albamu yenye ina nyimbo za kuvuma !!! Ndio nimesema .... LEO USIKU SAA 7 JIONI NAFICHUA JINA LA albamu 💽," Alisema Bahati.

Haya basi tunangoja, na mashabiki wanangoja kwa hamu kusikia jina la albamu hiyo na jinsi itakavyo kuwa.