Niko mahali nilipo kwa sababu ya Mungu-DJ Mo awashauri mashabiki

Muhtasari
  • Kila mtu ana hadithi yake mahali ametoka na mahali amefika sasa hasa kwa wale wamefanikiwa maishani
  •  
    Mo amebarikiwa na mke mmoja ambaye ni msanii wa nyimbo za injii Size 8 na watoto wawili
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwashauri mashabiki wake wasikate tamaa kwa ajili ya changamoto wanapitia kwani mahali alipo leo ni kwa ajili ya Mungu

Kila mtu ana hadithi yake mahali ametoka na mahali amefika sasa hasa kwa wale wamefanikiwa maishani.

Maisha ya watu wengi hayajakuwa rahisi wala hwajaamka siku moja na kujipata kuwa wana pesa, na wao ni mashuhuri, bali walitia bidii kayika kazi yao na kuwa mahali walipo leo.

Tunapozungumzia watu hao ni kama mcheza santuri DJ Mo ambaye ametoka mbali, kwa ajili ya bidii ya kazi yake.

Mo amebarikiwa na mke mmoja ambaye ni msanii wa nyimbo za injii Size 8 na watoto wawili.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwashauri mashabiki wake wasikate tamaa kwa ajili ya changamoto wanapitia kwani mahali alipo leo ni kwa ajili ya Mungu.

 

Niko mahali nilipo kwa sababu ya Mungu. Ninajimpenda - nimefanya kazi kwa bidii, nimejitolea sana bado siko mahali nataka lakini bado ninafanya kazi kuwa mahali ninapotaka kuwa. Wanaonijua, wanajua nimetoka mbali  ..yaani siku moja nitasimulia hadithi yangu. Kuwa na Msukumo na usikate tamaa hata iweje. … Nawapenda wote," Aliandika Mo.

Je hadithi yako ni ipi, au umepitia mambo yapi ili uwe mahai ulipo siku hii ya leo?