Ringtone amfokea msanii Bahati baada ya kupakia video akivuta sigara

Muhtasari
  • Ringtone amfokea msanii Bahati baada ya kupakia video akivuta sigara
Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Image: Hisani

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko mitandao ya kijamii Alimshambulia Bahati baada ya kushiriki video akivuta sigara.

Kulingana na Ringtone, alimuelezea Bahati kuwa mraibu wa dawa za kulevya.

Haya yanajiri saa chache baada ya Bahati kupakia video kwenye ukutasa wake wa instagram akivuta sigara.

Ringtone aliweka wazi kwamba kuwa yeye ndiye anaeza na kuelekeza tasnia ya burudani, na kuwa wasanii wa injili wanaendelea kutoa kibao baada ya kingine.

"Kutoka kuwa msanii wa nyimbo za injili hadi ukawa mraibu wa dawa za kulevya, lakini mimi ndio naendeleza tasnia ya burudani ya nyimbo za injili

lakini kila kitu kiko sawa, kwa maana tunato kibao kimoja baada ya kingine saa hizi #Fadia inafanya vyema kwenye youtube, wenye tunampenda Mungu tuendelee," Aliandika Ringtone.

Je ni vyema msanii Bahat kipakia video kama hiyo kwenye mitandao ya kijamii locha yake kuwa na wafuasi wengi mitandaoni?